Kozi hii inahusu uchafuzi wa mazingira na hewa, athari zake na jinsi ya kuzuia hali hiyo.
JoinKaribu watu wote duniani, asilimia 99 wanavuta hewa isiyo salama iliyopita viwango vya ubora wa hewa vilivyowekwa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na hivyo kutishia afya zao.
Hii inaathiri zaidi watoto kwakuwa bado wako katika hatua hatarishi ya makuzi. Ni vema kujiepusha na mazingira yoyote yenye hewa chafu ili kuwa salama.
Katika kozi hii utajifunza kuhusu uchafuzi wa hewa( ndani na nje), kujiepusha na hewa chafu, Mmomonyoko wa ardhi na jinsi ya kuzuia mazingira yasiharibiwe.
Kozi ni ya wiki mbili na ina vipengele vidogovidogo kwa kila wiki. Pia kuna video na viambatanisho vingine kwa ajili ya maelezo zaidi.