Kijana anayejitambua ni lazima ajue namna ya kuwajibika katika familia na jamii yake. Kozi hii inalenga kuhamasisha vijana kuchukua majukumu yao katika familia na jamii zao.
JoinKiana ni mwanafamilia na mwanajamii hivyo hawezi kukwepa kuwajibika sehemu zote hizo ili awe mtu wa manufaa. Kozi hii inalenga kuelezea familia na jamii kwa mtazamo wa Mungu na kuainisha majukumu mbalimbali katika taasisi hizo hasa kwa yanayohusu vijana.
Katika kozi hii utajifunza mada zifuatazo:
Mtazamo wa Mungu kuhusu Familia,
Majukumu katika familia na
Majukumu katika jamii.
Lengo kuu la kozi hii ni kujenga uwezo wa kijana katika kubaini majukumu yake na kuyafanya katika familia na jamii yake.
Kila mtu, haijalishi umri, ana jukumu na wajibu fulani katika familia na jamii. Katika kozi hii utahamasishwa kufikiri jinsi gani utachangia kwenye jamii yako ili kuleta mabadiliko chanya. Pamoja na mambo mengine heshima ya kijana inachangiwa na kuwajibika kwa bidii katika majukumu yake.
Fuatilia kozi hii hadi mwisho ili kufahamu zaidi kuhusu majukumu yako. Kutakuwa na viambatanisho mbalimbali pamoja na video zitakazokuwezesha kujifunza zaidi.
·
·