Mgawanyo wa majukumu ( Umri miaka 19-22) Compassion International | Hellen Willy |Tanzania

2 Weeks

Kozi hii inaelezea majukumu ya kijana katika familia na jamii.

Join

Heshima yako inatokana na jinsi unavyogusa maisha ya wengine.

Familia ni kikundi cha watu wanaokaa pamoja kama babamama na watoto. Kikundi hicho mara nyingi ni sehemu ya kundi kubwa zaidi la ukoo unaounganisha watu wenye asili katika uzao mmoja. 

Jamii ni watu wanaokaa pamoja na kushirikiana kwa mambo mbalimbali, kwa mfano masuala ya afya, elimu na ulinzi, mambo hayo yanapowakutanisha watu hujenga kitu kinachoitwa jamii, jamii hujenga umoja na upendo baina ya watu husika. bora inahitaji watu wenye upendo.

Watu wakipendana huweza kuishi na kujenga jamii bora, hivyo ni vyema watu wa sehemu husika wapendane ili waweze kujenga jamii ya namna hiyo. Pia katika jamii kila mmoja ana wajibu na majukumu ya kufanya mfano vijana, wazazi, wazee, viongozi n.k ili kuifanya jamii istawi.

Kozi hii inakutaka ufanye utafiti na kuweza kubaini majukumu na wajibu mbalimbali katika familia na kuweka mkakati wa kufanya shughuli za kuisaidia jamii yako.  Vilevile utajifunza mifano ya familia kutoka katika Biblia.

Syllabus

  • Majukumu ya kijana katika Jamii
  • Nguvu ya umoja katika Jamii.
  • Mambo ambayo jamii inayategemea kwa Kijana
  • Majukumu ya kijana katika familia
  • Mifano ya Famili kutoka katika Biblia
  • Familia za kawaida katika jamii yako
  • Mjadala kuhusu familia

When would you like to begin ?