MAJUKUMU YA KIJANA KATIKA FAMILIA NA JAMII ( Umri miaka 15-18) Compassion International | Hellen Willy |Tanzania

2 Weeks

Kijana anayejitambua ni lazima ajue namna ya kuwajibika katika familia na jamii yake. Kozi hii inalenga kuhamasisha vijana kuchukua majukumu yao katika familia na jamii zao.

Join

Ongeza maarifa kuhusu wajibu wako

Kiana ni mwanafamilia na mwanajamii hivyo hawezi kukwepa kuwajibika sehemu zote hizo ili awe mtu wa manufaa. Kozi hii inalenga kuelezea familia na jamii kwa mtazamo wa Mungu na kuainisha majukumu mbalimbali katika taasisi hizo hasa kwa yanayohusu vijana.

Katika kozi hii utajifunza mada zifuatazo:

Mtazamo wa Mungu kuhusu Familia,

Majukumu katika familia na

Majukumu katika jamii. 

Lengo kuu la kozi hii ni kujenga uwezo wa kijana katika kubaini majukumu yake na kuyafanya katika familia na jamii yake.

Kila mtu, haijalishi umri, ana jukumu na wajibu fulani katika familia na jamii. Katika kozi hii utahamasishwa kufikiri jinsi gani utachangia kwenye jamii yako ili kuleta mabadiliko chanya. Pamoja na mambo mengine heshima ya kijana inachangiwa na kuwajibika kwa bidii katika majukumu yake. 

Fuatilia kozi hii hadi mwisho ili kufahamu zaidi kuhusu majukumu yako. Kutakuwa na viambatanisho mbalimbali pamoja na video zitakazokuwezesha kujifunza zaidi. 

·        

·        

Assets

Syllabus

  • Majukumu katika Jamii kwa muktadha wa Biblia.
  • Unayo Fursa ya kuleta mabadiliko katika jamii yako
  • Shughuli za kijamii
  • Aina za familia
  • Mtazamo wa Mungu kuhusu Familia
  • Mjadala: Mtazamo wa Mungu kuhusu Familia
  • Kazi na Wajibu wa kijana katika Familia

When would you like to begin ?

Video Lectures